DAKIKA YA PILI TU CHOKORAA AFANYA ‘SUB’ MAPACHA WATATU


Hii unaweza kuifananisha na timu inayolazimika kubadilisha mchezaji dakika ya pili tu ya mchezo.

Bendi ya Mapacha Watatu chini ya Khalid Chokoraa, Jumapili ilishindwa kufanya onyesho lake Garden Breeze Magomeni kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali.

Mapacha Watatu ya Chokoraa ambayo ndiyo kwanza inaingia wiki ya pili tangu ijitupe sokoni, iliutangaza ukumbi wa Garden Breeze kama ukumbi wake wa nyumbani kwa kila Jumapili, lakini ikafanikiwa kufanya hivyo mara moja tu.

Khalid Chokoraa ameiambia Saluti5 kuwa mizengwe imekuwa mingi kwenye ukumbi huo sambamba na gharama za uendeshaji kuwa juu kuliko makubaliano ya awali yalivyokuwa na hivyo ameamua kuachana na ukumbi huo.

Chokoraa ameiambia Saluti5 kuwa wiki hii watatangaza ngome yao mpya ya kila Jumapili.

Wakati hayo yakitokea Garden Breeze, Chokoraa amesema onyesho lao la kila Jumamosi ndani ya Silver Sharks Kigamboni linakwenda vizuri.

No comments