DAR LIVE NDIYO HABARI YA ‘MUJINI’ LEO USIKU …Jahazi, Zanzibar Stars, Khadija Kopa ngoma nzito


Hatimaye siku imewadia, lile onyesho kubwa la muziki wa pwani lililokuwa linasubiriwa kwa hamu kubwa, linafanyika leo usiku ndani ya ukumbi wa Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Mlipuko wa burudani unategemewa kutokea katika onyesho hilo bab kubwa lililopewa jina la ‘Usiku wa kucharuka Kipwani na Singeli’.

Bendi za Jahazi Modern Taarab na Zanzibar Stars Modern Taarab zikirarajiwa kuchuana jukwaa moja huku pia kukiwa na burudani kutoka kwa Khadija Kopa, Khadija Yussuf, Hanifa Maulid, Dullah Makabila na Kivurande Junior.

No comments