DEBORAH AOTA KUFANYA KAZI NA GENEVIEVE NNAJ

MREMBO Deborah Ayolinde aliyehitimu mafunzo ya utayarishaji nchini Uingereza amesema kuwa anaota kuja kufanya kazi na Geneviene ambaye anafanya vizuri kwenye ulingo wa tasnia huko Nigeria.

Ayolinde alisema kuwa wapo mastaa wengi wanaofanya vizuri lakini kwake Genevive ndio chaguo la kwanza na ikiwa atapata nafasi ya kufanya nae kazi pamoja kwake itakuwa ni hatua kubwa.

“najua wapo mastaa kama Monalisa Chinda ambao navutiwa nao lakini kwasasa akili yangu inamuwaza Genevive” alisema staa huyo wakati wa mahojiano na jarida la Essence.


“Nahitaji kufanya nae kazi kwasababu najua kuna mambo mengi napaswa kujifunza kutoka kwake kwani ni muigizaji mzoefu ambaye amedumu kwenye fani kwa muda mrefu zaidi” alimaliza.

No comments