DIVA WA "ALA ZA ROHO" AWACHARUKIA WANAODAI YEYE NI "TEAM KIBA"

MTANGAZAJI wa kipindi cha "Ala za Roho" cha Clouds Fm, Diva amewacharukia vikali wale wanaodai yeye ni Team Kiba, baada ya kufanya mahojiano na mchekeshaji mama Ashura ambaye alitumia muda mwingi kuukosoa mwenendo wa Ali Kiba katika muziki wa sasa.

Diva amesema yeye hana timu na anaheshimu kazi yake na watu wanapaswa kuelewa kuwa kwa sasa yupo bize sana hawezi kushungulika na mambo kama hayo.

“Nimepata malalamiko, baadhi ya watu Oh kwanini umemualika Mama Ashura, wewe si Team Kiba, Oh Diva this and that. Naomba ni make it very clear mimi sina u team mambo ya u team yanagawa mashabiki wangu sitaki kwanza hata kusikia mambo hayo, tena Iam over that path. Mungu mwenyewe anajua nilivyo bize saa hii, building my life and future jamani, Have a lot in my plate, sahani yangu imejaa sana."

“Huo muda tena sina tena and Love everybody, yes. Napenda kila mtu hata Haters sababu wananifanya niwe famous, yes ila sichagui sibagui atakayenizika simjui, wanasema Waswahili. Mimi ninahudumia watu wote sihudumii pande moja tu, sitaki gawa mashabiki wangu kwa vitu ambavyo havinipi faida maishani, tuendeleeni kuwa mashabiki tuheshimiane,” ameandika Diva Instagram na kuongeza.


“Hivyo basi namualika yeyote kwenye show yangu nikijisikia na watu wakimuhitaji, sina pande yoyote ile, niko Busy nafanya kazi yangu na naheshimu sana kama ninavyoiheshimu serikali, nawapenda sana ila being Professional kumenipenda zaidi, I choose to be happy and means i “II support good mosic regaldress na ukinikosea Iam free shot you with nothing but the truth, I m free soul peace out,” amesisitiza.

No comments