DORTMUND YAKANUSHA TETESI ZA AUBAMEYANG KUDAIWA KUTAKA KUSEPA MAJIRA

TIMU ya Borussia Dortmund imezikanusha taarifa zinazodai kuwa nyota wao, Pierre Emerick Aubameyang akishindikana kuondoka majira haya ya joto, basi itakuwa ni Januari mwakani.

 Kwa sasa staa huyo anahusishwa na klabu za Chelsea na Paris Saint-Germains ama kusajiliwa kwa gharama kubwa na klabu za nchini China.


 Hata hivyo, jana Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Dortmund,  Hans-Joachim Watzke, alisema straika huyo raia wa Gabon ataendelea kuwatumikia miamba hao wa  Bundesliga.

No comments