FLOYD MAYWEATHER KUSUNDA DOLA MIL 300 DHIDI YA MCGREGOR

BONDIA Floyd Mayweather anatarajia kuingiza kitita cha dola za Marekani milioni 300, zaidi ya Sh bil. 664 za 
Tanzania, katika pambano lake dhidi ya Conor McGregor.

Kitita hicho ni sawa na Dola milioni 8 kwa kila dakika atakayokuwa ulingoni kuzichapa na mpinzani wake huyo.

Kutokana na mapato hayo, Mayweather amejitapa kuwa yeye ndiye mwanamichezo anayelipwa fedha nyingi duniani.
"Namaanisha, mimi ndiye mwanamichezo ninayelipwa fedha nyingi,” alisema mkali huyo.

Lakini pia, vyanzo mbalimbali vya mapato vimelitaja pambano lake na Conor litakalofanyika Agosti 26 kugharimu Dola za Marekani milioni 100.


No comments