Habari

FRANK LAMPARD AJIUNGA NA BT SPORTS KAMA MCHAMBUZI WA MICHEZO

on

NYOTA wa zamani wa soka wa klabu ya Chelsea, Frank Lampard,
amejiunga na BT Sports kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa michezo na anatarajia
kuanza kazi rasmi Jumapili hii kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Arsenal
dhidi ya Chelsea kwenye uwanja wa Wembley jijini London.
Mbali na mchezaji huyo, nyota huyo ataendelea kufanya hivyo
kwenye michuano mbalimbali ikiwa pamoja na Ligi Kuu nchini England, Kombe la
FA, Ligi ya Mabingwa Ulaya na michuano ya Kombe la Europa.
“Ninajisikia kuwa na furaha kubwa kujiunga na kituo hiki cha
uchambuzi cha BT Sport, tutakuwa Mubashara kwenye uwanja wa Wembley, Jumapili
hii katika mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Arsenal na Chelsea,” alisema
Lampard.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39, baada ya kumalizana na
klabu ya New York City mwaka jana, alifanikiwa kujiunga na kituo cha Sky Sports
kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *