GRAYSON SEMSEKWA ATIMKA TENA SKY MELODIES, NAFASI YAKE YACHUKULIWA NA FACEBOOK WA MASHUJAA


Rapa mwenye mwenye ‘madini’ mengi katika muziki wa dansi Grayson Semsekwa (pichani), anaingia kwenye orodha ya wasanii wenye historia ya kuhama hama bendi kila baada ya muda mfupi.

Hiyo ni baada ya kuondoka Sky Melodies ya Dodoma ambayo alikuwa anaitumikia kwa mara ya pili.

Nafasi ya Semsekwa aliyezitumikia pia bendi za Extra Bongo, African Revolution, Twanga Pepeta, Double M Sound na bendi kibao za mikoani, imechukuliwa na mwimbaji na rapa Facebook.

Bosi wa Sky Melodies Nicco Millimo  ameiambia Saluti5 kuwa Facebook aliyewahi kuitumikia Mashujaa Band, ameziba vizuri nafasi ya Semsekwa.

“Facebook ni rapa na mwimbaji mzuri, uwepo wake umeongeza changamoto kubwa kwa bendi za Dodoma,” anaeleza Nicco Millimo ambaye ni mwimbaji na mtunzi tegemeo wa Sky Melodies.


Mbali na Nicco Millimo na Facebook, waimbaji wengine wa Sky Melodies ni Alex Santah na Didier Namba huku Willy Bahari anayepiga solo na Joshcort Anelka anayepapasa kinanda nao pia wakiunda safu hiyo ya waimbaji.

No comments