Habari

HAJI MANARA ASEMA SIMBA ILICHEZA VIZURI JAPO ILIFUNGWA NA ORLANDO PIETES

on

VIGOGHO wa Soka Tanzania, Simba SC mapema wiki hii wamejikuta wakipoteza
mchezo wao wa kwanza wa kujipima nguvu katika kambi yao ya Afrika Kusini
kujiandaa na msimu mpya baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Orlando Pietes.
Kwa mujibu wa msemaji wa Simba SC, Hajji Sunday Manara Simba
inayofundishwa na kocha Mcameroon Joseph Omog ilicheza vizuri pamoja na kufungwa.
“Kwa mujibu wa maelezo ya benchi la ufundi mchezo ulikuwa mzuri
na timu ilicheza vizuri lakini bahati ilikuwa kwa wenyeji wao kupata ushindi huo,” amesema Manara.
Manara amesema Omog anayesaidiwa na Mganda Jackson Mayanja
aliwapa nafasi karibu wachezaji wote kucheza akipanga vikosi viwili tofauti
kila kipindi.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *