HAJI MANARA AWAPA SOMO VIONGOZI WAPYA WA TFF

RAIS mpya wa Shirikisho la Soka la Tanzania TFF, Wallace Karia na makamu wake, Michael Wambura, bado hawajaanza kuchanganya kutekeleza majukumu yao ndani ya ofisi za shirikisho hilo lakini Ofisa habari wa Simba, Haji Manara, ameamua kuwahi mapema na kuwauma sikio.

Manara amesema akina Karia ni lazima wajue Watanzania walikuwa wanakwazwa na kitu gani, kisha kuweka mambo sawa na kuhakikisha soka linachezwa kwa haki kwa kila mtu.

“Unajua TFF iligeuka kichaka hivyo viongozi wapya watambue fika Watanzania wameamka na wanataka haki ili soka lisonge mbele, vipaji vipo mikakati ndiyo inatakiwa ya kutufikisha mbali,” alisema.

Manara alisema Karia amepita kwa kishindo hiyo ni ishara ya kujua Watanzania wanahitaji awavushe hatua moja kwenda nyingine na kwamba ana mpango mzuri hasa uwazi wa mapato na matumizi.

“Kikubwa ni atimize kile ambacho alikiahido kwani mikataba yake ni wazi kwamba analitaka soka lisonge mbele,” alisema.


Karia amesema moja ya mambo atakayoyafanya ni kuboresha kamati ndani ya shirikisho hilo huku akiahidi matumizi na mapato ya TFF kuwekwa wazi.

No comments