Habari

HATIMAYE MOURINHO AKATA TAMAA YA KUSAJILI MCHEZAJI WA NNE MANCHESTER UNITED

on

Jose Mourinho amekiri kuwa huenda Manchester United isisajili mchezaji mwingine kiangazi hiki na sasa anajipanga na kikosi alicho nacho.
Mourinho bado anahitaji mshambuliaji wa pembeni licha ya kufanya usajili wa pauni milioni 146 kwa Romelu Lukaku, Nemanja Matic na Victor Lindelof.
Kocha huyo wa United amekuwa akihusishwa  kwa karibu na usajili wa   Ivan Perisic wa Inter Milan au Gareth Bale wa Real Madrid.
Lakini Mreno huyo amesema anaamini atalazimika kuridhika na wachezaji watatu aliowasajili kati ya wanne aliodhamiria kuwaongeza kwenye kikosi chake.
Alipoolizwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuhusu kusajili mchezaji wa nne, Mourinho alisema: “Sidhani kama tutaongeza mchezaji, labda litokee jambo lingine litakalotulazimisha kuingia sokoni.
“Nimemwambia (Mtendaji wa timu) Mr Woodward  kuwa malengo yangu yalikuwa wachezaji wanne, lakini pia nikamweleza asiwe na shaka, hakuna shinikizo kutoka kwangu, afanye kile ambacho anadhani ni sahihi kwa klabu.
“Tutakuwa pamoja tena kwenye dirisha lingine la usajili mwezi Januari au kiangazi kijacho hivyo hakuna ‘presha’ kabisa kutoka kwangu. Nipo tayari kwenda bila mchezaji wa wanne. Kama tuko nje ya sako sina tatizo, niko tayari”.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *