HATIMAYE ROBALDO AFIKISHWA KWA "PIRATO"

KESI inayomkabili  Cristiano Ronaldo imeanza kuunguruma baada ya juzi kutinga mahakamani mjini  Madrid kwa ajili ya kusomewa mashitaka ya awali kuhusu kashfa ya ukwepaji kodi inayomkabili.

Habari kutoka nchini humo zilieleza  jana kuwa straika huyo wa Real Madrid, ambaye anakana tuhuma hizo aliwasili kwenye mahakama ya  Pozuelo de Alarcon  ambayo ipo eneo anakoishi asubuhi ya jana hiyo kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.

Katika kesi hiyo waendesha mashitaka wanai kuwa staa huyo mwenye umri wa miaka 32  anadaiwa kukwepa kodi yenye ya Euro milioni 14.7 ambazo zilitokana na uuzaji wa hatimiliki ya picha zake.

Mshindi huyo  mara nne wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia  Ballon d'Or  anadaiwa kutenda kosa hilo mwaka  2010 na kuficha kiasi hicho kosa ambalo linakanwa na uongozi wa kampuni yake ya Gestifute.

Endapo  Ronaldo atakutwa na hatia katika kesi hiyo wataalamu wa  masuala ya kodi nchini humo wanasema kwamba anaweza kukabiliwa na fainali ya Euro milioni 28 ama kifungo cha miaka mitatu  na nusu jela.

Kesi hiyo ndiyo iliyozua kuhusu  hatima ya  Ronaldo kuendelea kuitumikia klabu yake baada ya kulalamika kuhusu kudukuliwa taarifa za ulipaji kodi wae, inagawa kwa sasa anaonekana ataendelea kubaki nchini humo.

No comments