Habari

HAYA NDIYO MAJINA YA VIGOGO WAPYA WA KAMATI ZOTE ZA TFF …Ally Mayai, Abbas Tarimba, Hanspope, Shaffi Dauda ndani

on

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia amewateua
Makamu wa Rais wa zamani wa TFF, Athuman Nyamlani na Ahmed Mgoyi kuwa Wajumbe
wa Kamati ya Utendaji ya TFF.
Rais Karia ameteua kwa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo katika Katiba
ya TFF ikiwa ni wiki moja baada ya kupatikana kwa viongozi wa shirikisho katika
uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 12, mwaka huu.
Rais Karia aliwatambulisha viongozi hao kwenye Kikao cha Kamati ya
Utendaji iliyofanyika Jumanne Agosti 22, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho pia Rais Karia alitumia fursa hiyo kutangaza
viongozi wa kamati mbalimbali za TFF zikiwamo za kinidhamu na kisheria.
Kamati ya Nidhamu: Mwenyekiti Tarimba Abbas, Makamu Mwenyekiti, Peter
Hella wakati wajumbe ni Boniface Lyamwike, Dk. Bill Haonga na Kassim Dau.
Kamati ya Rufani za Nidhamu: Mwenyekiti ni Wakili Rahim Zuber Shaban;
Makamu Mwenyekiti, Stella Mwakingwe wakati Wajumbe ni Abbas Mtemvu, Amani Mulika
na Siza Chenja.
Kamati ya Maadili: Mwenyekiti ni Wakili Hamidu Mbwezeleni, Makamu
Mwenyekiti ni Wakili Steven Zangira wakati Wajumbe ni Glorious Luoga, Walter
Lungu na Amin Bakhressa.
Kamati ya Rufaa ya Maadili: Mwenyekiti ni Wakili Ebenezer Mshana; Makamu
Mwenyekiti ni DCP. Mohammed Mpinga na wajumbe 
ni Wakili Benjamin Karume, George Mayawa na ASP. Benedict Nyagabona.
Kamati ya Uchaguzi: Mwenyekiti ni Revocatus Kuuli; Makamu Mwenyekiti
ni Wakili Mohammed Mchengerwa; Wakili Edwin Mgendera; Wakili Kiomoni Kibamba na
Wakili Thadeus Karua.
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi: Mwenyekiti ni Kenneth Mwenda; Makamu
Mwenyekiti ni Jabir Shekimweri na Wajumbe ni Wakili Rashid Sadalla, Irene
Kadushi na Mohammed Gombati.
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji: Mwenyekiti ni Elias
Mwanjala; Makamu Mwenyekiti ni Wakili Malangwe Mchungahela wakati Wajumbe ni
Zakaria Hanspope, Robert Selasela, Goodluck Moshi, Mhandisi Issa Batenga na
Hamis Semka.
Kamati ya Fedha na Mipango: Mwenyekiti ni Michael Wambura; Makamu Mwenyekiti
ni Francis Ndulane na Wajumbe ni Almas Kasongo, Pascal Kihanga, Maximillian
Tabonwa, Paul Bilabaye na Farid Abeid.
Kamati ya Mashindano: Mwenyekiti ni Ahmed Mgoyi; Makamu Mwenyekiti ni
James Mhagama wakati Wajumbe ni Kenneth Pesambili, Shafii Dauda, Fortunatus
Kalewa na Mhandisi Andrew Makota.
Kamati ya Ufundi: Mwenyekiti ni Vedastus Lufano; Makamu Mwenyekiti ni
Issa Bukuku na wajumbe ni Sarah Chao, Ally Mayay, Michael Bundala, Omar
Abdulkadir na Israel Mujuni.
Kamati ya Soka la Vijana: Mwenyekiti ni Khalid Abdallah; Makamu
Mwenyekiti ni Lameck Nyambaya na Wajumbe ni Mohammed Aden, Ramadhani Nassib,
Salim Kibwana na Vicent Majili.
Kamati ya Mpira wa Wanawake: Mwenyekiti ni Amina Karuma; Makamu
Mwenyekiti ni Rose Kissiwa na Katibu wa Kamati hiyo ni Somoe Ng’itu wakati
Wajumbe ni Zena Chande, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Zuhura Kapama na Nia
Mjengwa.
Kamati ya Waamuzi: Mwenyekiti ni Saloum Chama; Makamu Mwenyekiti
Joseph Mapunda wakati Wajumbe ni Nassib Mabrouk, Leslie Liunda na Soud Abdi.
Kamati ya Habari na Masoko: Mwenyekiti ni Dunstan Mkundi; Makamu
Mwenyekiti ni Mbasha Matutu wakati Wajumbe ni Imani Kajura, Mgaya Kingoba,
Godfrey Dilunga na Samson Mbamba.
Kamati ya Ukaguzi wa Fedha: Mwenyekiti ni Yahya Hamad; Makamu
Mwenyekiti ni Athuman Nyamlani na Wajumbe ni Khalifa Mgonja, Japhary Kachenje,
Jackson Songoro na Benesta Rugora.
Kamati ya Tiba: Mwenyekiti ni Dkt. Paulo Marealle; Makamu Mwenyekiti
ni Dkt. Fred Limbanga Wakati wajumbe ni Dkt. Norman Sabun, Dkt. Lisobina
Kisongo, Dkt. Eliezer Ndalama, Dkt. Elson Maeja na Violet Lupondo.
Kamati ya Futsal na Beach Soccer: Mwenyekiti ni Ahmed Mgoyi; Makamu
Mwenyekiti ni Hussein Mwamba na Wajumbe ni Blassy Kiondo, Isaac Munisi, Didas
Zimbihile na Aaron Nyanda.
Kamati ya Ajira: Mwenyekiti ni Issa Bukuku; Makamu Mwenyekiti ni
Saloum Chama wakati Wajumbe ni Athuman Kihamia, Mtemi Ramadhani, Noel Kazimoto
na Hawa Mniga.
Kamati ya Leseni za Klabu: Mwenyekiti ni Wakili Lloyd Nchunga; Makamu
Mwenyekiti Wakili Emmanuel Matondo wakati Wajumbe ni Profesa Mshindo Msolla,
Hamisi Kissiwa na David Kivembele.
Kamati ya Rufaa za Leseni: Mwenyekiti Wakili Dk. Damas Ndumbaro;
Makamu Mwenyekiti ni Wakili Alex Mngongolwa Wajumbe ni Meneja wa zamani wa
Uwanja wa Taifa, Charles Matoke, Tumainiel Mlango na Ahmed Menye.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *