Kutoka pande za Dodoma, mkali wa dansi wa anga hizo, Hussein Yamodo (pichani juu) anashuka na wimbo mpya kabisa unaokwenda kwa jina la “Hao”.

Yamodo ambaye ni star wa bendi ya Saki Stars ya Dodoma, ameiambia Saluti5 kuwa kazi hiyo itapenyezwa kwenye vituo vya radio ndani ya siku chache zijazo.

Mwimbaji huyo amesema mbali na “Hao” pia ana nyimbo nyingine mbili mpya ambazo nazo ziko mbioni kuachiwa hewani.

“Nataka kutoa jumla ya nyimbo tatu ndani ya mwezi mmoja lakini kila wimbo utakuwa kwenye staili tofauti,” alisema Yamodo.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac