IBRAHIMOVIC NI KAMA VILE HATAKI KUONDOKA MANCHESTER UNITED

STRAIKA aliyemwagana na Manchester United, Zlatan Ibrahimovic, huenda akarejea tena kukipiga na klabu hiyo ya Old Trafford, baada ya kuonekana kutokuwa na mpango wa kwenda kucheza katika michuano ya Ligi Kuu ya Marekani, MLS.

Rais wa Klabu ya Los Angeles Galaxy, Chris Klein, alisema walikuwa wakitaka kumsajili nyota huyo, lakini wameshindwa baada ya kuona hana mwelekeo na sasa huenda akasajiliwa tena na Manchester United.

No comments