Habari

IJUE VIZURI ‘DIMBA MUSIC CONCERT’ ITAKAYOKUTANISHA NYOTA WA DANSI SEPTEMBA 2 TRAVERTINE HOTEL

on

Kampuni ya New Habari (2006) LTD kupitia gazeti lake la DIMBA,
imeandaa onesho maalum la muziki wa dansi DIMBA Music Concert litakaofanyika
Septemba 2 mwaka huu katika Ukumbi wa Traventine Magomeni jijini Dar es Salaam.
Onesho hilo lina lengo la kuukuza na kupromoti muziki wa dansi, ambao
umekuwa ukielekea kupotea kila kukicha.
Katika onesho hilo kutakuwepo na mpambano wa wanamuziki wa dansi,
ambapo bendi ya Msondo Ngoma Music (Baba wa Muziki), itachuana na mastaa
mbalimbali wa muziki huo kutoka bendi mbalimbali nchini.
Kundi la mastaa ambao tumewapa jina la ‘Timu ya Taifa ya Muziki wa
Dansi,’ litakalochuana na Msondo Ngoma, litaundwa na wanamuziki kama Kikumbi
Mwanza Mpango’ King Kiki’, Hassan Rehani Bitchuka ‘Stereo’, Karama Regesu, Ally
Choky, Juma Kakere, Nyoshi El-Saadat ‘Sauti ya Simba’ na Muumini Mwinjuma.
Kwa upande wa vyombo, watakuwepo wapiga vyombo Saadi Ally ‘Machine’
kwenye dramu, gitaa la solo likitekenywa na Aldofu Mbinga wakati besi
litangurumishwa na Hosea Mhogachi.
Aidha, kinanda kitatekenywa Juma Jerry wakati tumba zitakung’utwa
Salum Chakuku ‘Kuku Tumba’, ambapo ala za upepo watakuwepo Ally Yahaya, Hamis
Mnyupe Tarumbeta na Shaabani Lendi kwenye Saksafoni.
“Utakua ni usiku wa mastaa wa dansi kuionyesha kazi Msondo Ngoma,
kwani miaka ya hivi karibuni imekua ikikosa mbabe katika kila bendi
inayoshindanishwa nayo lakini safari hii tumeamua tuwaonyeshe kazi.”
Kiingilio katika onesho hilo litakaloanza kuanzia saa 2:00 usiku hadi
majogoo, kitakuwa ni shilingi 10,000 kwa wote na 20,000/- kwa VIP.
IMETOLEWA NA MENEJA WA TUKIO ‘DIMBA MUSIC CONCERT’ MWANI NYANGASSA

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *