ISHA MASHAUZI AINGIA STUDIO KUPAKUA “THAMANI YA MAMA” …kitu kipya cha taarab


Isha Mashauzi ameingia studio kurekodi wimbo mpya wa taarab akiwa na bendi yake ya Mashauzi Classic.

Wimbo unakwenda kwa jina la “Thamani ya Mama” ambao tayari uliishaanza kuteka mashabiki kwenye kumbi mbalimbali inapopiga Mashauzi Classic.

Studio inayohusika na upikaji wa wimbo huo mpya wa Isha Mashauzi ni Sound Crafters chini ya producer Enrico.

Wimbo huu ni mwendelezo wa Isha Mashauzi wa kuonyesha namna anavyomthamini mama yake.

Ni wimbo wenye mashairi matamu yanayosisitiza umuhimu  wa mama na bila shaka utakuwa zawadi nzuri kwa kila anayemthamini mama yake.

Isha Mashauzi ameiambia Saluti5 kuwa wimbo huo wa taarab utakuwa hewani ndani ya siku chache zijazo.

No comments