IVORY BAND YAITIKISA JIJI LA MWANZA …"Shika Moyo" yaacha gumzo


Ivory Band ya Dar es Salaam, imefanya kweli jijini Mwanza kwa kukandamiza show za nguvu ndani ya ukumbi wa Villa Park.

Bendi hiyo inayoongozwa na waimbaji Saleh Kupaza, Rama Pentagon pamoja na mpiga kinanda Omar Kisila, ilianza kushambulia jukwaa la Villa Park tangu siku ya Alhamisi, katika mkataba wao wa show za siku nne mfulilizo hadi Jumapili August 13.

Wakitumia mfumo wa kupiga nyimbo mchanganyiko za kwao na za kunakili, Ivory Band wakafanikiwa kuwafanya mashabiki wasibanduke kwenye ‘dancing floor’.

Mwimbaji pekee wa kike wa bendi hiyo Amina Juma, alikuwa kivutio kwa namna alivyokuwa anatiririka vizuri na sauti yake tamu, huku wimbo wao mpya “Shika Moyo” ukiacha gumzo kubwa.

Wimbo huo ulikuwa ukiombwa na mashabiki mara kwa mara na kulazimika kupigwa kwa zaidi ya mara tatu katika kila show.

Pata picha kadhaa za onyesho la Ivory Band Ijumaa usiku ndani ya Villa Park.
Hapa mwimbaji Rama Pentagon (kushoto)  akionyesha uwezo wa kupiga gitaa la bass huku mpiga bass Seba akiwa kwenye kinanda
Amina Juma mwimbaji pekee wa kike wa Ivory Band
 Rashid Sumuni akicharaza solo gitaa
 Saleh Kupaza akitupia masauti yake
 Mkongwe Benno Villa akisalimia kisanii show ya Ivory Band
Wakazi wa Mwanza wakisataga ngoma za Ivory Band
Makamuzi yakiendelea 
Mpiga kinanda Omar Kisila naye akilisabahi gitaa la bass
No comments