J-LO ASEMA ANAVUTIWA NA MISOSI ANAYOKARANGIZA MWENYEWE NA SIO POMBE

STAA  mwenye mvuto wa kimapenzi Duniani, Jennifer Lopez amesema kuwa yeye sio muumini wa pombe bali anavutiwa zaidi na ulaji wa chakula alichotengeneza kwa mkono wake mwenyewe.

Akizungumza na Paper Magazine, staa huyo amesema kuwa kuna wakati huwa anatumia mvinyo kiasi kwasababu ya afya lakini kwake chakula ni jambo la msingi zaidi.

“Watu hawanifahamu vizuri mimi huwa sichezi kamari na kunywa pombe usiku, napenda chakula kilichotokana na mkono wangu mwenyewe,” alisema staa huyo.


“Natumia muda mwingi kwenye kazi za sanaa na jikoni kwasababu sipendi chakula cha kununua, kwa sasa mimi ni mzazi siwezi tena kuishi maisha ya zamani,” alimaliza.

No comments