JAHAZI KUANGUSHA SHOW YA NANE NANE MPO AFRIKA TANDIKA LEO USIKU


Kundi la Jahazi Modern Taarab leo usiku litaangusha show ya kukata na shoka ndani ya ukumbi wa Mpo Afrika, Tandika jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa viongozi wa Jahazi, Prince Amigo, ameiambia Saluti5 kuwa show hiyo ni maalum kwaajili ya kusherehekea sikukuu ya Nane Nane.

Miongoni mwa nyimbo za Jahazi zinazotegemewa kuitikisa Mpo Afrika ni pamoja na zile mbili mpya “Nataka Jibu” na “Jicho la Mungu Halilali” ambazo kwa sasa ndiyo habari ya mjini.

No comments