JAHAZI MODERN TAARAB KULA IDDI EL HAJJ MTWARA …Idd Pili wako Masasi, Idd Tatu Lindi


Kundi namba moja la muziki wa taarab, Jahazi Modern Taarab “Wana wa Nakshi Nakshi”, limeweka hadharani ratiba yake ya sikukuu ya Eid Hajj.

Kiongozi wa kundi hilo, Prince Amigo ameiambia Saluti5 kuwa Idd Mosi Jahazi watakuwa mjini Mtwara katika ukumbi wa Peninsula Hotel.

Kwa mujibu wa Amigo, Idd Pili inayotarajiwa kuwa Septemba 2, Jahazi watakuwa Masasi katika ukumbi wa BR.

Idd Tatu Jahazi watarindima Lindi ndani ya See View Beach Resort.

No comments