JAHAZI, YAH TMK, WAKALI WAO NANI ZAIDI? …ni Jumapili hii Travertine Hotel


Bendi tatu za taarab zenye bifu na zenye rekodi ya kuporana wasanii – Jahazi Modern Taarab, Yah TMK na Wakali Wao, zitaumana jukwaa moja Jumapili hii.

Itakuwa ni ndani ya ukumbi wa Travertine Hotel Magomeni, jijini Dar es Salaam ambapo itatafutwa ni bendi gani kali zaidi.

Jahazi ambayo ndiyo iliyopelekea kuzaliwa kwa Yah TMK, kisha ikapelekea kusukwa upya kwa bendi ya Wakali Wao, itakuwa na kazi kubwa ya kuthibitisha kuwa yenyewe ndio baba ya bendi hizo mbili.

Viongozi wa bendi zote tatu wameiambia Saluti5 kuwa hakuna udugu wala kujuana katika onyesho hilo, ni mpambano wa kushikishana adabu na kubwa zaidi ni kwamba onyesho ni moja tu, hakuna onyesho la marudiano wala la kujiuliza

No comments