JOAO MARIO AMTAKA RENATO SANCHES AONDOKE INTER MILAN NA KUTUA AC MILAN

STAA wa timu ya Inter Milan, Joao Mario amemtaka kiungo wa  Bayern Munich, Renato Sanches  kuachana na klabu hiyo ili akajiunge na mahasimu waoa katika jiji la Milan, timu ya  AC Milan.

Sanches  kwa sasa anajiandaa kuwatema mabingwa hao wa ligi ya Bundesliga, bada ya kushindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika msimu wake wa kwanza kuichezea klabu hiyo ya  Allianz Arena, baada ya kuwasili  kwa ada ya Euro milioni 35 akitokea Benfica.

Awali Bayern walikuwa wakionesha dalili za kwamba wangemruhusu akacheze kwa mkopo, lakini baada ya kung’ara katika mchezo wao dhidi ya  Chelsea wanaonekana kubadili mawazo na AC Milan ndiyo klabu ambayo inaonekana kummezea mate.

Kutokana na hali hiyo, Joao Mario  ambaye timu yake ya Inter wiki iliyopita waliichapa Bayern  mabao 2-0  anaamini kuwa klabu hiyo ya  San Siro ndipo mahali pazuri kwa ajili ya nyota mwenzake huyo.

"Tulizungumza Alhamis  wiki iliyopita baada ya mechi ," staa huyo aliliambia jarida la  Gazzetta dello Sport. "Bado ni kijana na anapenda kucheza hilo nalifahamu,” aliongeza.

“Nilimwambia aende AC Milan atakuwa amejiunga na klabu kubwa  na nitakuwa na moja wa marafiki zangu katika mji huu wa Milan,”aliongeza tena staa huyo.

No comments