JOH MAKINI APANIA KUFUNIKA KIMATAIFA

MSANII wa muziki wa kundi la "Weusi", Joh Makini amesema mipango yake ni kuhakikisha anafanya kazi bora zaidi zitakazoweza kumtangaza kimataifa.

Makini ambaye hivi sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa "Kata Leta" aliomshirikisha msanii kutoka Nigeria Davido, alisema ili msanii aweze kufanikiwa lazima ajitangaze kwa kufanya kazi zenye ubora.

Alisema tasnia nzima ya muziki kwa sasa imeonyesha ushindani wa hali ya juu, si kwa wasanii Watanzania tu hata wale wa nje ya nchi.

“Mipango yangu ni kufanya kazi bora zaidi na zaidi, hivyo mara baada ya kuachia "Kata Leta" kazi nyingine kali zitafuata."

“Nimegundua ili uweze kujitangaza lazima uvuke mipaka ya Tanzania kutafuta wasanii wakubwa wa kimataifa ambao wamekuwa wakifanya vizuri na kuwashirikisha kwenye kazi zako,” alisema Makini.


Msanii huyo hadi sasa amefanikiwa kuwashirikisha wasanii watatu wa kimatifa katika kazi zake tofauti, ambao baadhi yao ni Chidinma na Aka.

No comments