JOHN TERRY AKUMBUKA "NYUMBANI"... awatembelea wachezaji wenzake wa zamani wa Chelsea mazoezini

BEKI  na nahodha wa zamani wa Chelsea, John Terry ni kama amekumbuka nyumbani baada ya kuwatembelea wachezaji wenzake wa zamani wakati wakiwa mazoezini kwenye uwanja wao wa  Cobham.

Terry aliagwa kwa heshima na klabu hiyo ya  Blues mwishoni mwa msimu uliopita ikiwa ni baada ya kuitumikia timu hiyo kwa muda wa miaka 19.

 Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, staa huyo mwenye umri wa miaka  36  ambaye anakipiga kwenye klabu ya  Aston Villa alifanya ziara hiyo juzi  na kupokelewa kwa furaha na nyota hao wenzake wa zamani  na kisha akapiga picha nao.


Miongoni mwa wachezaji wa Chelsea aliopiga naoa picha ni pamoja na winga  Pedro ambaye baadae alitupia picha hiyo kwenye mtandao wake wa  Instagram ikiwa na ujumbe usemao ni vizuri tumekutana  tena na wewe mkongwe.

No comments