JOSE MOURINHO AWAPIGA KIJEMBE CHELSEA

SI unajua Jose Mourinho na Chelsea picha haziendi kabisa tangu alipoondoka Stamford Bridge?

Si unajua mastaa wa Chelsea walihusishwa sana na matokeo ya kutimuliwa kwake klabuni hapo, akiwamo Eden Hazard. 

Basi bana, kwa sasa ukiwa ni msimu wake wa pili Manchester United, Mreno huyo amewarushia kijembe mastaa wake wa zamani.

Unajua amesema nini, Mourinho ambaye hivi karibuni alimsajili Nemanja Matic Chelsea alisema kikosi chake cha sasa huko Manchester United kina wachezaji bora na ndicho bora zaidi alichowahi kufanya nacho kazi tangu aanze ukocha.

Kwenye msimu wake wa kwanza huko Man United, Mourinho aliishia nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu England licha ya kunyakua mataji matatu, ngao ya jamii, Kombe la Ligi na Europa League.

Hata hivyo, kwa sasa baada ya kuwanasa wachezaji kadhaa ikiwemo Romelu Lukaku, Paul Pogba, Matic, Victor Lindelof, Henrinkh Mkhitatyan, Mourinho anaamini ana kikosi matata kabisa kuwahi kukinoa.


“Nina furaha kweli kweli kwa kuwa kocha wa wachezaji hawa, sijawahi kuwa na kundi la wachezaji walio vizuri zaidi kama hawa katika maisha tangu ya ukocha,” alisema Mourinho na kuongeza: “Nitapambana kwa ajili yao.”

No comments