JOSE MOURINHO BADO ANAMPIGIA HESABU IVAN PERISIC


Jose Mourinho bado anamtaka Ivan Perisic kutoka Inter Milan ili kuweka uwiano mzuri kwenye kikosi chake cha Manchester United.

Mourinho anamuona winga huyo mwenye umri wa miaka 28 kama mtu pekee atakayeweza kuifanya safu ya ushambuliaji ya Manchester United iwe tishio.

Bado bodi ya Manchester United imeshindwa kufikia bei ya pauni milioni 48 iliyowekwa na Inter Milan na sasa kuna tishio la Chelsea kuingilia kati dili hilo.


No comments