JUMA KATUNDU ‘AFUKIA’ SAUTI YA DEDE MSONDO NGOMA


Wengi wamekuwa wakijiuliza Msondo Ngoma itakuwa vipi baada ya mwimbaji mkongwe Shaaban Dede kufariki dunia, lakini maswali hayo yanajibiwa vizuri kwa vitendo na mwimbaji ‘kiraka’ Juma Katundu (pichani juu).

Juma Katundu ndiye anayefukia mashimo kuziba pengo la sauti ya Shaaban Dede na alianza kuifanya kazi hiyo kiufasaha hata kabla Dede hajafariki.

Katika maonyesho mengi yaliyofanyika wakati Dede akiwa mgonjwa, ni Juma Katundu ndiye aliyekuwa akiimba vipande vyote vya Dede.

Katundu ambaye pia ni bingwa wa kuziba sauti za waimbaji kadhaa waliopita Msondo Ngoma, anamudu vipande vyote vilivyoimbwa na Dede katika nyimbo zote – mpya na za zamani.

No comments