JUUKO MURSHID KUTUA YANGA DIRISHA DOGO LA MWEZI DESEMBA

YANGA inataka kuimarisha safu yao ya ulinzi na katika mpango huo wamefichua kwamba watamchukua beki wa Simba, Juuko Murshid.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba Juuko ambaye amebakiza miezi mitatu katika mkataba wake na Simba ameona ni vigumu kwa klabu yake hiyo kukaa meza moja kumalizana na Yanga na kwamba ameihakikishia hataongeza mkataba wa kuendelea na timu hiyo.

Bosi mmoja wa Yanga amesema baada ya majaribio ya beki huyo kujiunga na klabu moja nchini Afrika Kusini hataki kurudi Simba na sasa anataka kuondoka ambapo atabaki Msimbazi kwa miezi mitatu ili kumalizia mkataba wake.

Bosi huyo amesema tayari wameshamsainisha beki huyo kwa mkataba wa awali ambapo mara baada ya mkataba wake kumalizika atajiunga na Yanga mwezi Desemba akiingia katika usajili wa dirisha dogo.

“Juuko hataki kabisa kucheza Simba baada ya kushindwa kujiunga na timu ya Afrika Kusini ambapo kumemuumiza sana na ametuambia anakuja kutufanyia kazi kubwa,” alisema bosi huyo.


“Tumeshamweka sawa na amekubali kuingia mkataba wa awali na klabu yetu, tunawahakikishia mashabiki na wanachama wetu kuwa Juuko atatua klabuni Desemba na tunachotaka ni kuwa na beki imara katika mechi za Ligi ya Mabingwa, kikosi cha Ligi ya ndani tunacho.

No comments