JUVENTUS YAITUPILIAMBALI OFA YA CHELSEA KWA ALEX SANDRO

KLABU ya Chelsea bado inahaha kuboresha kikosi chake baada ya kupeleka ofa ya pauni mil 63 kwa Juventus ili kumsajili Alex Sandro ofa ambayo imekataliwa.

Chelsea wapo kwenye wakati mgumu kukisuka kikosi chao baada ya kupoteza Nemanja Matic huku pia Costa akigoma kurudi kambini.


Klabu ya Juventus nayo imeweka wazi kuwa haina mpango wa kuachana na staa wake huyo katika dirisha hili la usajili.

No comments