KABAMBA TSHISHIMBI NI SOO MAZOEZINI YANGA

KIUNGO mpya wa Yanga, Kabamba Tshishimbi ameanza kuonyesha uwezo mkubwa katika kikosi hicho akifanya kweli katika majukumu yake lakini akawashtua wengi kufanikiwa kufunga bao akiwa mazoezini.

Akiwa katika mazoezi yake ya kwanza tu unaambiwa Tshishimbi amefanikiwa kutuliza mzuka wa makocha wa Yanga akionyesha uwezo mkubwa wa kukaba kwa nguvu na kuanzisha mashambulizi.

Achanma na hayo yote, kifaa hicho kutoka DRC Congo akafanya makubwa baada ya kufunga bao malidadi katika mazoezi yake ya kwanza, taarifa ambazo hazitawavutia mashabiki wa Simba waliodhani jamaa hatotua nchini.

Katika mchezo wa juzi Tshishimbi alionekana kuwa imara na kuimarisha safu ya kuingo ya timu hiyo ambapo tayari makocha wameonyesha kukubali uwezo wake hatua ambayo ni wazi watamuingiza katika kikosi cha kwanza.

Wakati mambo yakienda hivyo, matajiri wa Yanga wametua Pemba tayari kwa kazi ya kupandisha morali kwa wachezaji hao wakianza kwa kuwajaza noti mifukoni tena hata kabla ya mchezo.


Vigogi hao wa kamati ya mashindano wakiongozwa na mwenyekiti wao, Majid Seleman wametua kambi ya Pemba ambapo mbali na kuwajaza mamilioni, tayari wamemwambia kila mmoja akirudi akaangalie akaunti yake ya benki na kwamba tayari mishahara yao imeshaingizwa ili akili zao zitulie kummaliza mnyama.

No comments