KAGERA SUGAR KUWEKA KAMBI BURUNDI

KIKOSI cha timu ya soka ya Kagera Sugar kinatarajia kuweka kambi nchini Burundi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaoanza Agosti 26, mwaka huu.

 Kagera ambayo ilianza maandalizi yake kwa kuweka kambi ya wiki mbili jijini Dar es Salaam, kwa sasa ipo mkoani Kagera, ikiendelea na mazoezi kabla ya kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Singida United na Yanga.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Mecky Mexime, amesema baada ya mechi hizo watajiandaa na safari ya kwenda Burundi, ambako watakaa wiki moja na kucheza mechi za kirafiki kabla ya kurejea.

“Naamini michezo ya kirafiki itatuweka kwenye taswira mpya ya mwonekano na kikosi chetu msimu ujao utakuwa tofauti na tutafanya vyema,” alisema.


Mexime, ambaye aliiwezesha Kagera kumaliza Ligi Kuu msimu uliopita ikiwa nafasi ya tatu, ameahidi kuendeleza makali yake msimu ujao.

No comments