KANYE WEST ATAMBULISHA BIASHARA YA VIATU GHALI ZAIDI

MKALI wa Hip Hop, Kanye West, ametambulisha viatu vyake vipya huku pea moja itakuwa ikiuzwa dola za Kimarekani 300 sawa na sh 655 500 za Kitanzania.

Mbali na viatu hivyo aina ya raba ambavyo pia vitakuwa vikitofautiana bei, staa huyo atakuwa na tisheti na kofia.

Hata hivyo viatu hivyo vitaanza kuuzwa Novemba mosi, mwaka huu.


Taarifa za ujio wa bidhaa hizo sokoni hazikutolewa mapema ingawa kuna kumbukumbu nzuri kuwa West alianza kuvivaa tangu Februari.

No comments