KATIE PRICE MBIONI KUVUNJA NDOA YAKE YA TATU

STAA Katie Price ameripotiwa kuwa mbioni kutaka kuvunja ndoa yake na Kieran Hayler ambaye ni mume wake wa tatu.

Kabla ya kuwa na Kieran Hayler, Katie alishawahi kufunga ndoa na Peter Andre kisha wakatengana na baadaye kufunga ndoa na Alex Reis ambayo hata hivyo haikudumu muda mrefu.

Imeripotiwa kuwa Katie hana furaha na ndoa yake baada ya kubaini kuendeleza michepuko na sasa wamefika hatua ya kutaka kutalikiana.

Huu ni mwendelezo wa matukio ya ndoa za mastaa nchini Marekani ambapo wengi wao wamekuwa na mahusiano ya muda  mfupi kama ilivyo kwa Jennifer Lopez ambaye amekuwa na kasumba ya kubadili wanaume kila baada ya muda mfupi.

No comments