KICGHUYA ASEMA HAJAONA WA KUGOMBANIA NAE NAMBA NA KUMWEKA KWENYE WAKATI MGUMU SIMBA

WINGA wa Simba, Shiza Ramadhan Kichuya amekiangalia kikosi cha timu yake msimu ujao na kusema hakuna mchezaji wa kumweka benchi.

Katika kikosi cha Simba, Kichuya anayecheza winga ya kulia au kushoto anawania namba na mchezaji Mohamed Ibrahimu "MO", Jamali Mnyate na muda mwingine Emmanuel Okwi ambaye anacheza pia kwenye nafasi ya ushambuliaji.

Akizungumza, Kichuya amesema kuwa hadi hivi sasa hajaona mchezaji anayeweza kugombania naye namba na kumpa wakati mgumu.

“Wapo wachezaji ninaocheza nao namba moja lakini nikiwaangalia hakuna anyeweza kuniweka benchi kutokana na kiwango chake kunizidi,” amesema.


“Nitakaa benchi kwa kupata majeraha au kuumwa lakini si kwa kuzidiwa uwezo na hili linatokana na mimi mwenyewe kupigana kwa hali na mali kuhakikisha muda wote ninakuwa fiti na nikipata nafasi ya kuingia uwanjani sifanyi makosa kwani nahitaji kuona kocha hanitoi kwenye kikosi chake cha kwanza.”

No comments