Habari

KIPA WA CHELSEA ASEMA PENGO LA SANCHEZ LINAZIBIKA ARSENAL

on

KIPA wa Chelsea,
Thibaut Courtois, amesisitiza kwamba Klabu ya Arsenal inaweza kuachana na nyota
wake, Alexis Sanchez, kwa kuwa pengo lake linaweza kuzibika.
Courtois anaamini
kuwa Arsenal wana wachezaji wengi wazuri ambao kwa ubora wao wanaweza kutumika
kuziba pengo la nyota huyo raia wa Chile.
Nyota huyo
anafukuziwa na klabu ya Manchester City pamoja na Paris Saint Germain (PSG), ambayo
ipo tayari kutoa kitita cha pauni milioni 35 ili kuinasa saini yake.
Inadaiwa kuwa,
Sanchez ana mpango wa kuhamia Manchester City, lakini huenda akabadili uamuzi
huo endapo PSG watakuwa na mpango wa dhati kwa kuzidisha ada ya usajili.
Sanchez (28), hakuwa
katika kikosi cha Arsenal kilichocheza kwenye michuano ya Kombe la Emirates
wiki iliyopita, ambapo kwenye posti yake ya Istagram alidai sababu za
kukosekana alikuwa mgonjwa.
Kutokuwapo kwake
kumepunguza kidogo hali ya msuguano kuhusu hatima yake, huku kocha wa timu
hiyo, Arsene Wenger, akisisitiza kwamba nyota wake huyo hauzwi.
Mshambuliaji
huyo, ambaye amefikisha mabao 72 katika kikosi cha Arsenal, anaweza kumaliza
utata uliopo kwa kulazimisha usajili wa kwenda Manchester City.
Alipoulizwa
kuhusu Sanchez, Courtois alilieleza gazeti la Evening Standard kuwa Sanchez ni
mchezaji bora kutokana na michezo yake aliyocheza msimu uliopita alionesha
ubora mkubwa sana.
“Sanchez ni
mchezaji hodari mwenye uwezo mkubwa katika soka, mwepesi na mwenye mbinu, ni
mchezaji muhimu kwao, lakini Arsenal wana wachezaji wenye ubora zaidi.
“Watamkumbuka,
lakini nafikiri wanaweza kupata mbadala bora zaidi yake na kwa kuwa tayari
wamefanya usajili mzuri wa mshambuliaji,” alisema Courtois.

Courtois, ambaye
atakuwa kipa katika mchezo wa Kombe la Ngao ya Jamii dhidi ya Arsenal wiki
ijayo, aliongeza kuwa angependa Sanchez asiwepo kwenye mchezo huo kutokana na
ubora wake.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *