Habari

KIPA YOUTHE ROSTAND AIPONDA SIMBA SC NA KUIITA “YA KAWAIDA SANA”

on

KIPA
namba moja wa Yanga ambaye juzi alifanya kazi nzuri ya kuokoa michomo ya Simba,
Youthe Rostand raia wa Cameroon amesema kuwa wapinzani wao ni wa kawaida sana
tofauti na ilivyokuwa ikielezwa kwenye vyombo vya habari.
Kipa
huyo ambaye alipangua penalti ya Shabalala amesema kuwa haoni kama Simba
inaweza kuwa kikwazo kwao kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo
inatarajia kuanza kutumia vumbi kesho Jumamosi.
“Huu
ni mchezo wangu wa kwanza mkubwa tangu nifike hapa nchini lakini kwa jinsi
nilivyoitazama Simba sioni kwamba ni timu inayoweza kuwa kikwazo kwetu kutetea
taji,” amesema kipa huyo.
“Unaweza
kuona namna tulivyowadhibiti kuanza mwanzo wa mchezo hadi dakika ya mwisho,
suala la penalti linajulikana kwasababu katika hatua hiyo jambo lolote linaweza
kutokea uwanjani,” aliongeza.
Kiwango
cha kipa huyo katika mchezo huo pia kilikuwa gumzo kwa mashabiki ambao tayari
wameonekana kuanza kumsahau Dida aliyetimkia Afrika Kusini kucheza soka la
kulipwa.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *