Habari

KIPIGO CHA SIMBA DHIDI YA ORLANDO CHAMFUNZA JOSEPH OMOG

on

KOCHA wa Simba, Joseph Omog amesema baada ya timu yake kucheza
mechi ya kwanza ya kirafiki Jumatano hii na kufungwa bao 1-0, ameanza kuona
mwanga wa kupata kikosi kipya cha kwanza cha wachezaji 11.
Hii ni wiki ya pili sasa Simba imepiga kambi nchini Afrika Kusini ikijifua kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku
lengo kubwa kwa kocha wao huyo raia wa Cameroon likiwa ni kutwaa taji ambalo linashikiliwa
na mahasimu wao Yanga.
 Akizungumza kutoka Johannesburg, kocha Omog alisema mechi hiyo ndiyo iliyompa
taswira kamili ya ubora wa kikosi chake baada ya kufanya mazoezi magumu kwa
muda wote ambao wapo nchini humo.
“Nimependekeza kucheza na timu hii kwa sababu ndiyo
kipimo kizuri kwa mazeozi ambayo tumeyafanya hapa nchini lakini kitu kikubwa
kwangu sio kuangalia matokeo bali ninachotaka kuona ni namna gani wachezaji
wameyashika yale tuliyoyafundisha na jinsi wanavyoyafanyia kazi,” alisema Omog.
Omog alisema kwa maandalizi waliyoyafanya anaamini msimu ujao
watakuwa ni moja ya timu inayopigania ubingwa wa Ligi ya Bara na anawashukuru
viongozi kwa kuwapa maandalizi mazuri ya sasa kazi imebaki kwao kurudisha
shukrani kwa kutwaa mataji yote ambayo wanagombania.
Kikosi cha Simba kinatarajia kurejea nchini Agosti 6 na siku
mbili baadaye kitashuka kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam kupambana na
Rayon Sports ikiwa ni siku maalum kwa timu hiyo (Simba Day), ambayo hufanyika
kila mwaka huku dhumuni lake kubwa likiwa ni kutambulisha wachezaji wapya pamoja na jezi.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *