KLOPP AJIPA MATUMAINI YA KUNYANYUA KOMBE LA LIGI KUU ENGLAND MSIMU HUU

KOCHA wa  Liverpool, Jurgen Klopp anasema kuwa kikosi chake kinaweza kutwaa taji la michuano ya Ligi Kuu England, baada ya kushindwa kufanya hivyo msimu uliopita.

 Liverpool ilianza msimu wa 2016-17 vizuri na walikuwa pointi sita pekee nyuma ya viongozi na hatimaye bingwa wa ligi Chelsea  hadi Januari mwaka huu.

Lakini walirudi nyuma baada ya kupata ushindi mmoja mwezi Januari na Februari kabla ya kumaliza katika nafasi ya nne pointi 17 nyuma ya Chelsea.

''Tutashiriki mechi za ubingwa.hatutaki kuanza msimu bila kuwa na lengo lolote'', alisema Klopp.

"Lazima tuwe na lengo na nadhani tuna timu nzuri sana sasa.tulikuwa na bahati mbaya msimu uliopita''.


''Nadhani tunaweza kucheza vyema .Tuwe na matumaini kwamba kila kitu kitakuwa shwari. Klop alisema kuwa kwamba mchezaji Phillipe Coutinho hauzwi, licha ya Barcelona kumtaka'',”aliongeza kocha huyo.

No comments