KOCHA CONTE ASEMA HANA WASIWASI KUWAKOSA WACHEZAJI WAPYA WALIOWATARAJIA

KOCHA wa Chelsea Antonio Conte anasema hana wasiwasi kufuatia kushindwa kwa klabu hiyo kuwasaini wachezaji wapya msimu huu.

Chelsea amewasaini wachezaji wanne kwa jumla ya pauni mil 129, lakini wachezaji wengi walihama klabu hiyo wakiwemo John Terry na Nemanja Matic.

 “Klabu inajaribu kila iliwezalo,” alisema Conte.

Sambamba na beki wao, John Terry na mchezaji wa kiungo wa kati Matic, Chelsea wamemuuza Amir Begovic kwenda Bournemouth huku mfungaji bora wa msimu uliopita Diego Costa ameambiwa kuwa yuko huru kuondoka klabu hiyo.

Kusainiwa kwa wachezaji wa kiungo wa kati Tiemoue Bakayoko kutua Monaco, mshambuliaji Alvaro Morata kutoka Real Madrid, mlinzi Antonio Rudiger kutoka Roma na aliyekuwa kipa wa Manchester City Willy Caballero, kujaza pengo lililoachwa wazi.


Hata hivyo Conte ameweka wazi mipango yake ya kusaini wachezaji zaidi ili kuboresha kikosi chake kwa msimu huu.

No comments