KOCHA JACKSON MAYANJA AWATOA HOFU WANASIMBA JUU YA KIKOSI CHAO

KOCHA msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema kwamba wanachama  na mashabiki wa klabu hiyo hawana sababu ya kuwa na wasiwasi na kikosi chao.

Mganda huyo amesema kwamba baadhi ya mashabiki wamekuwa na wasiwasi kutokana na washambuliaji wao kukosa mabao katika baadhi ya mechi, lakini amesema kwamba tatizo hilo limefanyiwa kazi.

Kocha huyo amesema kwamba ni kweli wamekuwa na tatizo la umaliziaji katika Simba, lakini mapungufu hayo yamefanyiwa kazi na wekundu hao watapata matokeo mazuri katika mechi zinazowaabili.

“Kumekuwa na tatizo la umaliziaji katika timu yetu, lakini tumekaa na kufanya marekebisho ambayo tunaamini kuwa yatatupa matokeo mazuri,” amesema.

Simba kesho Jumatano watakabiliwa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga kwenye uwanja wa Taifa, kuashiria kuanza kwa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.


Wekundu hao wako katika kambi ya mazoezi mjini Zanzibar wakati Yanga wamejificha kisiwani Pemba.

No comments