KOCHA LWANDAMINA AITENGENEZA YANGA MPYA KWA AJILI YA SIMBA SC

YANGA ipo tayari mwanangu asikwambie mtu na taarifa zilizowashtua Simba ni juu ya safu ya ushambuliaji wa timu hiyo ambayo haikauki mabao.

Taarifa kutoka kambi ya Pemba ni kwamba kocha George Lwandamina amemaliza kazi ya kukisuka kikosi hicho ambapo safu hiyo ya ushambuliaji imekuwa na mabadiliko makubwa.

Lwandamina amepanga kuwatumia washambuliaji wawili wanaohofiwa vikali na Simba ambao ni Donald Ngoma na Ibrahim Ajib huku kushoto akitoka Emanuel Martin ambaye amekuwa mtamu kuliko asali wakati kulia akimpa jukumu mkongwe Thabani Kamusoko.

Utamu zaidi kwa Yanga ni katika safu ya kiungo ambapo ingizo jipya Kabamba Tshishimbi atakuwa ndani ya nyumba huku juu yake akipewa jukumu mtaalam Raphael Daud Kuwalisha washambuliaji.

Licha ya Kamusoko kupangwa kama kiungo wa pembeni lakini amewapa jukumu la kuja kukaba kati akisaidiana na Tshishimbi na Raphael hatua ambayo itawasumbua zaidi Simba.


Lwandamina ambaye amewabadilisha vilivyo wachezaji wake wakionekana kuimarika katika stamina na pumzi ambapo jambo la hatari zaidi kwa Simba ni juu ya uwezo mkubwa wa kukaba na kutengeneza mashambulizi.

No comments