KOCHA WA JUVENTUS AKANA TETESI ZA ALEX SANDRO KUWA MBIONI KUJIUNGA NA CHELSEA

KOCHA wa Juventus,  Massimiliano Allegri amekana kuhusu tetesi zilizosambaa zikidai kuwa nyota wake, Alex Sandro atakwenda kujiunga na  Chelsea akisisitza kwamba raia huyo wa Brazil hataondoka kwenye klabu hiyo ya vinga vya Turin.


Juzi Alex Sandro alicheza muda wa dakika  45 katika mchezo ambao Juve waliambulia kipigo cha mabao  2-0  dhidi ya Tottenham kikiwa ni cha pili  kukipata katika michezo yao  ya kujiandaa na msimu ujao.

No comments