KOCHA WA MONACO AFUNGUKA CHANZO CHA MBAPPE KUSUGUA BENCHI

UONGOZI wa klabu ya AS Monaco unaonekana kuamua kumsulubu straika wao Kylian Mbappe, baada ya kocha wake Leonardo Fardim kusema kuwa ndio ulioamua amsugulishe benchi wakati wa mechi yao ya majuzi ambayo waliibuka na ushindi dhidi ya Dijon, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ufaransa League 1.

Katika mchezo ambao mabingwa hao watetezi waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 ambao umewafanya kuwa na mwanzo mzuri kinda huyo alikuwa amekaa benchi akiwashuhudia wenzake uwanjani.

Mbappe alikumbwa na majeraha wiki iliyopita wakati wa mchezo ambao waliibukana ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Touleuse na hakuweza kupangwa tena katika mchezo wa kuwania kombe la Stade Gaston Gerard, ambao Radamel Falcao aliweza kupiga ‘hat trick’ na hjku Jemerson akipiga bao moja.

Kutopangwa kwa nyota huyo kumeanza kuzua tetesi kuhusu hatima yake na huku timu ya PSG ikilipotiwa kuwa mbioni kumpeleka Parc des Princens.

Hata hivyo pamoja na tetesi hizo Jardim alisema juzi kuwa nimuhimu kumpa mchezaji kupumzika kwa baadhi ya mechi kabla ya michuano ya ligi ya Mabingwa hatua ya makundi kuanza septemba mwaka huu.

“Ni uamuzi wa klabu ambao umeamua tusimpange katika mechi za mwanzo za ligi,” Jardim aliwaambia weaandishi wa habari.


“Na kwaupande mwingine wakati mechi zinapokuwa bado sio ngumu, kunaulazima wa kuwapa nafasi wachezaji wengine iliniweze kujenga kikosi imala ,” aliongeza kocha huyo.

No comments