KOCHA WA PANONE FC ACHUKUA MIKOBA YA ALLY BUSHIR MWADUI YA SHINYANGA


ALIYEKUWA kocha wa Panone FC, Jumanne Ntambi amejiunga na Mwadui FC kuchukua nafasi ya Ali Bushir aliyetupiwa virago.

Ntambi aliyewahi kuifundisha Mwadui miaka ya nyuma, amesaini mkataba wa kukinoa kikosi hicho kwa msimu ujao.

Katibu mkuu wa Mwadui, Ramadhani Kilao alisema Kocha huyo ataungana na Khalid Adam aliyekuwa kocha msaidizi wa Julio na Bushir.

Alisema kuwa kati ya makocha hao, baada ya kusaini mkataba wanaangalia nani atakuwa kocha mkuu kwa sababu wote wanalingana kiwango cha elimu ambacho ni leseni ‘B’.


“Baada ya kumuondoa Bushir tumemleta kocha mwingine anaitwa Ntambi, anaendelea na mazoezi na timu lakini kesho (juzi), ndio atasaini mkataba ila tutaangalia nani atakuwa kocha mkuu yeye na Khalid,” alisema Kilao.

No comments