KUZIONA SIMBA NA YANGA NGAO YA JAMII NI BUKU SABA TU

MAANDALIZI ya mchezo wa ngao ya jamii utakaowakutanisha mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2016/16, Young Africans na Mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sport Federation Cup) Simba inakwenda vyema.

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), limeutangazia umma kuwa viingilio katika mchezo huo vimepangwa katika makundi manne, ambapo sehemu ya VIP ‘A’ tiketi zake ni sh 25,000.

VIP ‘B’ na ‘C’ sh 20,000, viti vya rangi ya chungwa sh 10,000 na mzunguko kwa vitu vya rangi za bluu na kijani ni sh 7,000.


Tiketi zimeanza kuuzwa jana Jumanne, Agosti 15, 2017 ili  kuwapa fursa wadau wa mpira wa miguu kununua tiketi mapema kujiepusha na usumbufu.

No comments