LEBRON JAMES: ANAYEUKARIBIA UBORA WA MICHAEL JODAN NI KOBE BRYANT, SIO MIMI

WAKATI mashabiki wengi wa mpira wa kikapu wakijua LeBron James ndiye anayekaribia ubora wa Michael Jordan, mkongwe huyo amekanusha, huku akimtaja Kobe Bryant.

Jordan amedai kuwa, Kobe ni habari nyingine, na wala hawezi kusita kutamka hadharani kuwa LeBron anasubiri kwa mshikaji huyo.

"Ningemtaja LeBron kuwa bora kuliko Kobe katika ishu ya mchezaji bora wa muda wote? Hapana. Kwa sasa (LeBron) anaweza kuwa bora, lakini Kobe alishinda mataji matano. LeBron ana mawili."


Jordan ametoa maoni yake hayo, licha ya kujua wazi kuwa James ameshinda tuzo nne za Mchezaji Bora (MVP), lakini Kobe ameichukua mara moja.

No comments