LESASA JOCKER AISHIKA DUBAI NA BENDI YAKE YA BILENGE MUSICA INTERNATIONAL


Pichani ni Captain Lesasa Jocker, kiongozi wa Bilenge Musica International yenye maskani yake Dubai ambapo hutumbuiza Rush Inn Hotel Club Africana kila wiki.

Kwa zaidi ya miaka 20, Jocker amekuwa akifanya muziki huko Dubai na hivi karibuni anatarajiwa kuzindua album yake mpya “MILELO”.

Lesasa mzaliwa wa Congo, pia alipiga muziki Kenya kwa miaka mingi na kupata umaarufu mkubwa sambamba na kuibua na kuvilea vipaji vya wanamuziki wengi.

Kila mwaka, wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, Lesasa na bendi yake huwa wanarejea Kenya kwa mapumziko ya mwezi mzima.

Imeandikwa na Prince Kinmedia, Nairobi - Kenya

No comments