Habari

LIGI KUU SASA TIMU 20, TIMU 6 KUPANDA DARAJA, MBILI ZITASHUKA 2018/19

on

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
litapandisha idadi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu msimu ujao wa 2018/19 kutoka
16 za sasa hadi 20, imefahamika.
Uamuzi huo umefanyika Jumanne Agosti 22, 2017 wakati Kamati ya
Utendaji inafanya marekebisho ya Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza inayotarajiwa
kuanza Septemba 16, mwaka huu.
Kwa marekebisho hayo, timu zitakazoshuka daraja msimu ujao kutoka Ligi
Kuu ya Vodacom ya sasa ni mbili hivyo kubaki 14. Na ili kufikia timu 20, timu
sita (6) za Ligi Daraja la Kwanza zitapanda daraja.
Kwa mujibu wa utaratibu wa Ligi Daraja la Kwanza,  ina maana
kwamba msimu huu timu mbili zitapanda kutoka katika kila kundi katika ligi hiyo
ambayo inatarajiwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.
Makundi ya Daraja, kundi ‘A’ lina timu za African Lyon, Ashanti
United, Friends Rangers za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani,
Mgambo JKT ya Tanga, Mvuvumwa ya Kigoma na Polisi Moro ya Morogoro.
Kundi ‘B’ ziko za Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya
Dar es Salam, Mawezi Market ya Morogoro, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi United
ya Iringa, Mshikamano na Polisi Dar za Dar es Salaam.
Kundi ‘C’ lina timu za Alliance School, Pamba na TotoAfrican za Mwanza, Rihno Rangers ya 
Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma, Transit Camp ya
Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *