LIONEL MESSI AMTAKIA NEYMAR KILA LA KHERI PSG


Lionel Messi ni kama vile ameshakubali kuwa safari ya Neymar kujiunga na Paris Saint-Germain haizuliki ambapo kupitia Instagram ameandika salam za kumtakia nyota huyo wa Brazil kila kheri.

Neymar alitumia dakika 43 tu kwenye mazoezi ya Barcelona mapema leo na kuwaaga wachezaji wenzake ikiaminika kuwa anajiunga na PSG kwa pauni milioni 198.

Messi akaweka video iliyosindikizwa na maandishi yaliyosema: "Ilikuwa ni heshima kubwa sana kushirikiana na wewe rafiki yangu (Neymar) kwa miaka yote hiyo, nakutakia kila la kheri katika hatua yako mpya ya maisha".No comments